Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Clifford Mario Ndimbo ameelzea maandalizi ya timu ya taifa “Taifa Stars” ambayo imeingia kambini tarehe 21 Agosti, kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu CHAN dhidi ya Uganda utakaopigwa mwezi huu tarehe 28 Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Ndimbo, Clifford Ndimbo: Maandalizi yamekamilika, Watanzania Wajitokeze kwa Wingi, Meridianbet

Ndimbo amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia zote,k na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo huo.

“Maandalizi yamekamilika kwa asilimia zote, Watanzania tujitokeze kwa wingi kwenda kuwaunga mkono Taifa Stars kwenye mchezo wa kuwania kufuzu CHAN dhidi ya Uganda August 28”

Ndimbo, Clifford Ndimbo: Maandalizi yamekamilika, Watanzania Wajitokeze kwa Wingi, Meridianbet

Stars chini ya kocha Kim Poulsen hii leo wameendelea na mazoezi katika uwanja wa Mkapa huku wachezaji wote 25 walioitwa wakiwa wamefika kambini, huku mchezaji wa Azam FC Tepsie Evance nae akiwa sehemu ya kikosi hicho na amefanya mazoezi pamoja na wenzake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa