Cole Palmer Anaendelea Alipoishia

Cole Palmer ameendelea alipoishia msimu uliomalizika kwani moto wake unaoneokana kuendelea kuwaka ambapo kwenye mchezo wa leo amefanikiwa kuhakikisha alama zote tatu klabu yake ya Chelsea wanazipata dhidi ya Brighton.

Kiungo Cole Palmer amefanikiwa kufunga mabao manne leo katika ushindi wa mabao manne ambao klabu yake ya Chelsea wameupata dhidi ya Brighton katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza, Hii inaonesha kwa namna gani mchezaji huyo amekua na mwendelezo wa kiwango bora mpaka sasa tangu ajiunge na klabu ya Chelsea.cole palmerRaia huyo wa kimataifa wa Uingereza leo amefanikiwa kuingia kwenye vitabu vya historia kwakua mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne kipindi cha kwanza katika historia ya ligi kuu ya Uingereza, Kwani mchezaji huyo mabao yake yote katika mchezo wa leo aliyafunga kipindi cha kwanza.

Mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kuchezwa michezo sita kiungo Cole Palmer tayari amehusika kwenye magoli 10, Akiwa amefunga mabao sita huku akiwa amepiga pasi nne zilizosaidia upatikanaji wa mabao jambo ambalo linamfanya kua mchezaji alihusika kwenye mabao mengi mpaka sasa msimu huu.

Acha ujumbe