Nyota wa Bayern Munich Kingsley Coman kukabiliwa na faini ya kuendesha gari ya McLaren badala ya Audi.
Mabingwa wa soka la Ujerumani, Bayern Munich wanadhaminiwa na kampuni ya kutengeneza magari ya Audi na watengenezaji hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa magari mapya kwa kila mchezaji tangu mwaka 2002.
Wachezaji wa Bayern wanapaswa kutumia magari ya Audi kila wanapokwenda mazoezini au kwenye shughuli rasmi za klabu kama sehemu ya mkataba. Lakini sasa kijana Coman amejiweka katika maji ya moto baada ya kuwa mchezaji wa hivi karibuni kuvunja sheria hiyo.
Ameingia mazoezini akiwa kwenye gari lake la McLaren Spider 570S na sasa atakabiliwa na faini na adhabu kutoka kwenye klabu.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kupigwa faini ya £170,000 baada ya mkurugenzi wa michezo Hasan Salihamidzic kuonya wachezaji kuwa atatoa adhabu kwa wale wasiofuata sheria za klabu.
Hivi karibuni, Nyota wengine wa Bayern Philippe Coutinho na Niklas Sule pia wameonekana wakiendesha gari zisizo za Audi.
Mfaransa huyo ameomba msamaha kwa kuendesha gari yake McLaren badala ya Audi yake.
“Ningependa kuomba msamaha kwa klabu na kampuni ya Audi kwa kufika mazoezi katika gari langu na sio la kampuni,” alisema.
“Sababu ilikuwa kioo cha Audi yangu kuharibiwa. Bado, hata hivyo naweza kuona nimefanya makosa.
“Kama fidia, nitatembelea kiwanda cha Audi huko Ingolstadt kwa saa moja mapema haraka na kusaini Autograph, kwa wafanyakazi wa kiwanda kizima.” Ikumbukwe Audi wamekuwa wazamini wa Bayern Munich tangu mwaka 2002 na wana mkataba ambao unaisha mwaka 2029 lakini pia kampuni hii ya magari ina share ya Asilimia 8.33 kwenye klabu.
Furahav
Duuh noma sana.