Inaonekana sasa tatizo limepata msuluhishaji ndani ya kikosi cha Inter Milan baada ya kuwa na misimu kadhaa isiyokuwa na mvuto kabisa ndani kikosi hicho chenye historia kubwa sana ndani ya soka. Klabu hiyo imeweza kuchezewa na majina ya pekee sana na pia imeweza kufundishwa na makocha wenye hadhi kubwa sana lakini ilionekana kuyumba kwa kipindi fulani na kuanza kuwa nje kidogo ya mvuto wa kupendwa sana na wengi kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa msimu huu linapotajwa jina Inter imekuwa na heshima kidogo kuwa ni klabu inayoonekana kuanza kujengeka kwa kiasi chake na kuonesha ushirikiano. Rekodi iliyosukwa tena na Conte ni ule ushindi ambao ameweza kuuweka katika klabu hiyo pale San Siro mbele ya kikosi bora kabisa cha Lazio ambapo amechukua alama zote 3 mbele yao na kumfanya kuweka rekodi ya kushinda mechi 5 mfululizo za ligi yao hiyo ya Italia.
Wenyeji hao, katika mechi yao ya watani iliyopigwa hivi karibuni, waliibuka na ushindi wa magoli 2 – 0 ambapo waliwatawala kwa mengi sana AC Milan ambao mara nyingi wamekuwa ndiyo wapinzani wake wa muda mrefu jambo ambalo kwa hakika ni rekodi ya pekee sana kimafanikio kwa kocha huyo mpya kikosini hapo.
Matokeo yalidumu hadi mwisho wa mechi hiyo ambapo Lazio walishindwa kutumia nafasi ya pekee waliyoipata kupitia Joaquin Correa na kushindwa kuzitumia mbele ya Handanovic ambaye alisimama imara katika milingoti yake mitatu ili kuwazuia kabisa Lazio wasitingishe nyavu zake.
Ushindi wao huo wa 5 kati ya mechi 5 walizocheza ni picha ya wazi kwamba watakuwa washindani wakubwa sana wa Juventus msimu huu mara baada ya kuonekana wana uwezo wa kufanya maamuzi ya kimatokeo wakati wowote wa mechi jambo ambalo ni zuri katika ligi hasa wanapopatikana wapinzani wa aina yake
Kwa sasa macho yake yapo kwa Sampdoria na baadaye atakapokutana na Barcelona kwenye mechi nyingine ambayo itaweza kuonesha endapo wamerudi au bado ni katika kujipanga na hicho huenda kikawa ni kipimo bora kwa Conte. Wakati mpinzani wake Lazio atakuwa na mechi zake nyumbani ambazo atapigana dhidi ya Genoa na Rennes.
Ester
Conte ni hatari sana