Meneja wa Tottenham, Antonio Conte amesisitiza umuhimu wa winga Steven Bergwijn katika mipango yake baada ya kufunga mara mbili akitokea benchi na kuwapa Spurs ushindi.
Umuhimu wa muholanzi huyo ulikuwa katika mashaka pale tottenham na kuvutia vilabu vya Ajax na Sevilla katika dirisha hili. Spurs walikataa dau la £15m kutoka Ajax kwaajili ya Bergwijn.
Bergwijn aliingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya Sergio Reguilon kabla ya kuifungia Tottenham bao la kusawazisha dakika ya 90+5 na kuongeza bao la ushindi dakika ya 90+7.
“Tangu mwanzo mtu aliniuliza kuhusu Steven Bergwijn. Nilikuwa muwazi. Nilisema kwangu mimi ni mchezaji muhimu kwasababu ana ubunifu ambao katika kikosi chetu hatuna wachezaji wengi wa aina hiyo.” alisema Conte.
“Ni mzuri dhidi ya mtu kwa mtu, mzuri kushimshinda mpinzani. Anaweza kucheza kama mshambuliaji, anacheza namba 10 kwetu.
“Steven ni mchezaji mwenye nguvu yupo fiti, anawez kuanza mchezo au anaweza kutokea benchi na kubadili mchezo. Kwangu mimi nadhani ni mchezaji muhimu ana furaha na anafuraha kuichezea Tottenham.” aliongeza Conte.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA