Baada ya kutimuliwa kwa Jose Mourinho, ambaye tayari amepata kibarua huko Italia, safari ya Tottenham kumsaka meneja mpya imekwama kidogo baada ya mazungumzo na Antonio Conte kuvunjika Ijumaa.

Spurs, walimtimua Jose Mourinho mwezi Aprili, walikuwa kwenye mazungumzo ya kumleta meneja huyo wa zamani wa Chelsea huko kaskazini mwa London.

Lakini imefahamika kuwa madai fulani yaliyotolewa na meneja huyo wa miaka 51 yamekuwa magumu na sasa wataelekeza mawazo yao mahali pengine.

Conte, alitajwa kuwa na nafasi kubwa zaidi kufuatia kuondoka kwake Inter Milan wiki iliyopita, ambapo aliondoka kwa makubaliano ya pande zote baada ya kuwaongoza kutwaa taji lao la kwanza la Serie A tangu 2010.

Conte na Spurs, Mazungumzo Yavunjika
Antonio Conte

Rekodi yake inavutia, akiwa ameshinda pia Ligi ya Premia akiwa na Chelsea mnamo mwaka 2017, alitarajiwa kurejea Spurs kuungana na mkurugenzi wa Juventus Fabio Paraciti, ambaye anatajwa kuwa mbioni kujiunga na klabu hiyo.

Daniel Levy alisema alitaka klabu kurudi kwenye “DNA ya msingi” ya kilabu ambayo ilipotea wakati wa uteuzi wa Mourinho.

Ripoti zinasema Conte imekuwa changamoto kuona Conte akikidhi vigezo vya kujiunga na klabu hiyo kufuatia vipaumbele vyake alivyonavyo kwa sasa.

Paraciti anatarajiwa kuwasili Spurs, na kuwa sehemu ya muhimu ya kumtafuta meneja mpya kwa ajili ya klabu yake.

Spurs pia imetajwa kuwa kwenye mazungumzo na bosi wa zamani Mauricio Pochettino juu ya kurejea kwake baada ya takribani miezi 18 tu baada ya kufutwa kazi, lakini mwajiri wake wa sasa Paris St Germain alizuia kutoka na itakuwa ngumu kukamilisha suala hilo tena tena.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa