Kwa mujibu wa ripoti thabiti kutoka Sky na Foot Mercato, uhamisho wa beki chipukizi wa Werder Bremen, Karim Coulibaly, uko karibu kukamilika. Strasbourg wamekubali kulipa ada ya msingi ya €20m, huku bonasi zikifikia hadi €5m na Werder wakipata kipengele cha asilimia 10 ya mauzo ya baadaye.

Coulibaly, mwenye umri wa miaka 19, aling’aa msimu uliopita Bundesliga baada ya kuibuka kutoka akademi ya Hamburger SV na kupewa nafasi Bremen kutokana na matatizo ya kikosi. Alitumia nafasi hiyo ipasavyo, akicheza mechi 27 na kuonyesha uwezo mkubwa.
Mambo muhimu kuhusu uhamisho huo ni pamoja na ada ya uhamisho inayosemwa kuwa €20m + €5m bonasi, jumla €25m. Ndani ya historia ya Bremen haya yanakua ni mauzo ya pili ya thamani katika historia ya klabu, nyuma ya Diego (€27m kwenda Juventus 2009).
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Coulibaly anaonekana kama mshumaa wa matumaini kwa timu ya taifa ya Ujerumani (DFB). Amecheza kwenye timu za vijana wa Ujerumani tangu U17 na alicheza mechi ya kwanza U21 Machi 2026 dhidi ya Ireland Kaskazini. Hata hivyo, ana asili ya Ivory Coast na tayari amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kubadili uraia wa soka.

Werder sasa wana zaidi ya €40m mapato ya usajili msimu huu, na lengo lao ni kumchukua kiungo Cameron Puertas kwa mkataba wa kudumu kutoka Al-Qadsiah, baada ya mkopo wake kufanikiwa.



