Mlinda lango wa Real Madrid Thibaut Courtois anaamini kwa asilimia zote kuwa Eden Hazard atabaki klabuni hapo zaidi ya msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea amekuwa na mwanzo mgumu kwa miaka miwili katika mji mkuu wa Uhispania tangia alipojiunga na Real Madrid, akipata changamoto ya majeraha mengi yaliyomfanya ashiriki mechi 43 tu na kufunga matano kwa klabu.

Courtois: Nina Uhakika Hazard Atasalia Madrid
Thibaut Courtois (kushoto) na Eden Hazard (kulia)

Hazard amekuwa akihusishwa kuungana tena na Chelsea na kumalizana na changamoto za muda wake aliokuwa huko Bernabeu, lakini Thibaut hatarajii mwanatimu mwenzake kuondoka Madrid msimu huu wa joto.

“Ninauhakika 100% atasalia. Hataki kuhama. Ni waandishi wa habari wa Madrid tu ndio wanaandika juu ya nia ya kuondoka.”

 

-Courtois

Thibaut anasisitiza kuwa, Hazard anataka kupambana na kushinda akiwa na Real Madrid, bila kuwa na changamoto ya majeraha na kushinda mataji.


Thibaut Courtois na Eden Hazard
Thibaut Courtois na Eden Hazard

Hazard amekuwa akikosolewa zaidi tangia alipojiunga na Madrid kiwango chake kikionekana kushuka tofauti na alipokuwepo Chelsea.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA


3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa