Hii sasa inawezekana ikawa biashara nzuri sana upande wa Bayern Munich kutokana na kumnasa nyota huyo ambaye kwa upande fulani kiuchezaji anaendana kabisa na namna ligi ya taifa hilo inachezwa. Ina maana kwamba kimfumo nyota huyo anaweza kutosheleza mahitaji ya klabu.
Munich wamemnasa nyota huyo kwa mkopo lakini kukiwa na kipengele kwenye mazungumzo yao kinachozungumzia suala la kumsajili kama wataridhia kufanya hivyo. Hiyo ni nafasi ya pekee sana kwao na wanaweza kufanya hivyo baada ya kujiridhisha na uwezo wake mbali na kwamba nyota huyo siyo wa kubezwa.
Klabu kama Manchester United na Chelsea zilikuwa zikitajwa kutamani sana saini ya nyota huyo lakini bahati imewaangukia Bayern ambao wamefanikiwa kuonesha ushawishi ndani ya Barcelona na hata kumfanya mchezaji mwenyewe aweze kukubaliana kusaini kandarasi hapo.
Jukumu la Bayern Munich litakuwa ni kulipa sehemu tu ya fungu ikiwa kama ada kwa nyota huyo na siyo kulipa pesa yote. Jambo ambalo litakuwa na faida sana kwao. Kiasi cha £8.5m pekee kinatosha kabisa kuweza kumfanya kiungo huyo raia wa Brazil kuonesha makali yake ndani ya klabu yake hiyo mpya.
Ila kutokana na kipengele kinachowataka Bayern kumnunua kabisa nyota hiyo watatakiwa kulipa mshahara wa mchezaji huyo ambao wamekubaliana. Hilo litapelekea chachu ya kupunguza matumizi klabuni hapo pia, litampa nguvu nyota huyo kuamua kwa baadaye kama ataridhika kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Karl-Heinz anaonekana ni mwenye furaha sana baada ya kufanikiwa kuliwekea ulinzi suala hilo la kumnasa Coutinho kutokana na uhitaji wao wa siku nyingi kutaka kuwa na nyota huyo. Kwao anaona ni kama mafanikio makubwa sana na yaliyopitiliza lakini anasema mahusiano yao na Coutinho hayajaanza leo ila ni muendelezo tu.
Awali Coutinho alitaka kutumika kama chambo kwa klabu ya PSG kukiwa na lengo kwamba angeweza kutolewa huko na kiasi kingine cha pesa ili waweze kumnasa Neymar lakini nyota huyo hakuwa tayari kuondoka klabuni hapo kwa namna hiyo iliyokuwa inatazamiwa na klabu yake hiyo.
Msimu huu tutamshuhudia akiandika historia mpya ndani ya klabu yake hiyo mpya ya Bayern ambayo usajili wake umelenga zaidi katika makombe makubwa ya Ulaya.
Hope mwaikuka
🙌