Cristian Ansaldi: Nitacheza Mpaka Miaka 40

Beki kisiki wa klabu ya Torino inayoshiriki ligi kuu ya Itali aCristian Ansaldi ana amini anaweza kucheza soka mpaka atakapo fika umri wa miaka 40, Beki huyo wa kushoto wa Argentina amejiunga na Torino kwa mkopo wa miaka miwili mwezi wa nane 2017 na kuwashawishi wakali hao wa Italia kutumia pauni milioni 2.5 kumsaljiri kwa mkataba wa kudumu mwezi Julai mwaka 2019.

Cristian Ansaldi

Mkataba huo unakadiriwa kuisha mwaka ujao lakini Beki huyo anaamini anaweza kukomaa na kibarua chake kwa miaka mingi zaidi kwenye timu hiyo. ” nafurahia kua hapa watu wananipenda na kila kitu kinaenda sawa unapokua na timu nzuri kwenye mji kama huu” alisema Cristian Ansaldi akizungumza na Angelo Maugeri kwenye ukurasa wake wa Instagram. “Uwezo wangu unakua msimu mmoja mpaka mwingine ni kwa imani tuu , kama mungu ana taka na raisi wa timu Urbano Cairo ataniruhusu nibaki kilabuni nitacheza mpaka miaka 40”

Kwa sasa Ligi ya Italia imesitishwa kutokana na tatizo la Korona na kufanya wachezaji kua na kipindi kigumu.

Ansadi amecheza mechi 16 akiwa Torino kwa msimu huu, na kufunga magoli manne na kusababisha magoli mengine matatu kwa kutoa pasi za mwisho na kuifanya timu yake kua ya 15 kwenye msimamo wa ligi ya Italia.

 

 

 

 

 

3 Komentara

    Axante kwa taarifa

    Jibu

    Cheza tu inategemea na uwezo utakao kua nao utapofikisha umri huo

    Jibu

    Mungu akuepushe na majeraha utafika tu

    Jibu

Acha ujumbe