Tottenham Hotspurs wanaripotiwa kuwa karibu na usajili wa beki wa kati wa Atalanta Cristian Romero.
Kwa mujibu wa Skysports, Atalanta wanajiandaa kupokea ofa ya £42.7m ya kumsaini staa huyu mwenye miaka 23 huku kukiwa na uwezekano wa gharama ya dili hilo kupanda hadi £47m.
Taarifa zinasema kuwa Cristian Romero yupo tayari kuungana na Tottenham msimu huu wa uhamisho wa majira ya joto na anajiandaa kusafiri kuelekea London kwa ajili ya vipimo.
Ripoti inadai kuwa Atalanta pia hawapotezi mda kabisa kumtafuta mbadala wa Romero klabuni hapo na tayari wameshaanza mazungumzo ya kumsajili beki wa Juventus, Merih Demiral pamoja na nyota wa Lille, Sven Botman.
Cristian Romero alikuwa ni sehemu muhimu ya kikosi cha Atalanta msimu uliopita akitwaa taji kama mlinzi wa msimu wa Serie A, pia akiwasaidia Argentina kushinda Copa America mwezi uliopita.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!
Sania+mapua
Habari njema