Mchezaji nyota wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo siku ya jana amerejesha matumaini ya klabu hiyo kwa kuweza kuisaidi kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Norwich baada ya kuifungia goli tatu kwenye mchezo huo uliosha kwa 3-2.

Hat-trick ya mshabuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano imefufua tena matumaini ua kuwania nafasi nne za juu baada ya kupanda mpaka nafasi ya tano huku wakiwa nyuma ya alama tatu dhidi ya Tottenham anayeshika nafasi ya nne.

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wachambuzi kutaka Cristiano aachwe kwenye kikosi cha Man Utd na kupewa nafasi vijana zaidi, huku kukiwa na tetesi kuwa mwisho wa msimu anaweza kuondoka kwa kuwa ni moja ya wachezaji ambao watakuwa mizigo kwa klabu kutokana na kushindwa kufuzu ligi ya mabingwa.

Kocha mpya ajaye kwenye klabu hiyo Erik ten Hag amemuonyeshea njia ya kutokea nyota huyo. Erik ten Hag mpaka sasa hajafanikiwa kusaini mkataba wa awali na klabu hiyo licha kufanikiwa kufanya makubaliano ya mazungumzo.

Kwa sasa Cristiano Ronaldo ana miaka 37 huku kwenye mkataba wake kukiwa kumebaki mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo, uwezo wake wa kufunga hauna shaka japo kuna maneno ambayo yana zungumzwa kuhusu uwezo wake wa kusukuma timu kwa mashambulizi ya haraka na kushuka kwa kasi yake.

Ilikuweza kuchochea kasi yake na kupunguzia mzigo klabu ya Man Utd inapaswa kusajiri mchezaji ambaye atasaidiana nae au kutafuta mrithi wa muda mrefu wa kuchukua nafasi yake, ikiwa ataondoka majira ya kiangazi.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa