Ligi ya Mabingwa inaendelea kuweka rekodi mbalimbali katika ulimwengu wa soka. Mchezo wa Juventus vs Dynamo Kiev, umetumika kuweka rekodi ya Cristiano Ronaldo.

Cristiano Ronaldo alipachika goli katika dakika ya 57 kwenye ushindi wa 3-0 na goli hilo licha ya kuwapa ushindi Juve, lakini pia limeweka rekodi kwa mchezaji huyu kufikisha magoli 750 tangu ameanza kucheza soka.

Akiwa ni mshindi mara 5 wa tuzo ya Ballon d’Or, alipokuwa Madrid alifunga magoli 450 katika michezo 438, na wakati akiwa United, alifunga jumla ya magoli 118. Goli la jana dhidi ya Dynamo Kiev, ni goli lake la 75 akiwa na Juventus.

Kwa siku za karibuni, Ronaldo aliweka rekodi nyingine kwa kufikisha zaidi ya magoli 100 akiwa na timu ya Taifa ya Ureno. Idadi hii ya magoli inamfanya Ronaldo awe mchezaji wa 2 duniani nyuma ya Ali Daei wa Iran kama wachezaji wenye magoli mengi katika timu za taifa.

Cristiano Ronaldo, Cristiano Ronaldo Afikisha Magoli 750!, Meridianbet
Ronaldo Akishangilia Baada ya kupachika goli dhidi ya Dynamo Kiev

Mpaka sasa, Ronaldo anaendelea kutamba kama mfungaji wa muda wote wa Real Madrid akiwa amemzidi Raul kwa jumla ya magoli 127.

Baada ya kuweka rekodi hiyo, Cristiano Ronaldo aliwashukuru wachezaji wenzake, kocha na wapinzani wake kwa kuwa na mchango katika kufikia hatua hiyo.

Ronaldo alisema ” magoli 750, nyakati za furaha 750, nyuso 750 za furaha kwa mashabiki wetu. Ninawashukuru wachezaji na makocha wote ambao wamenisaidia kuifikia hii namba, ninawashukuru wapinzani wangu wote kwa kunifanya niongeze juhudi katika utendaji kazi wangu.”

Mchezo wa Juventus dhidi ya Torino wikiendi hii utakuwa ni safari nyingine ya Ronaldo kulitafuta goli la 751. Katika mechi 4 dhidi ya Torino, Ronaldo amefunga kwenye mechi 3.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Cristiano Ronaldo, Cristiano Ronaldo Afikisha Magoli 750!, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

26 MAONI

  1. Aaaah hongera yake ronaldo huyo Mimi ninamuita mlipiza visasa wa magoli huwa kama amepoteza kufunga goli ujue wakati mwingine itamlazimu apate goli ili atomize lengo lake la kucheka na nyavu

  2. Aaaah hongera yake ronaldo huyo Mimi ninamuita mlipiza visasa wa magoli huwa kama amepoteza kufunga goli ujue wakati mwingine itamlazimu apate goli ili atomize lengo lake la kucheka na nyavu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa