Mahambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo mpaka sasa hajawasili klabuni kwa ajiri ya mazoezi ya kujianda na safari za pre-season na mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu kuchelewa kwake kuwasiri.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa mwenye miaka 37 kutoka nchini Ureno aliwasilisha maombi rasmi ya kuomba kuruhusiwa kuwekwa sokoni kwenye dirisha la usajiri huu, lakini klabu ya Manchester haiko radhi kumuuza kwa sasa.

Cristiano Ronaldo, Cristiano Ronaldo Kutokuripoti ni Shinikizo Ili Auzwe?, Meridianbet

Cristiano Ronaldo kukosekana kwake mpaka sasa kunazua maswali mengi kwa kocha wake mpya Erik ten Hag. Klabu ya Manchester United kwa sasa inasubili maelezo ya CR7 sababu iliyomfanya asiweze kuwasiri kwa wakati.

Mpaka sasa haiko wazi, ikiwa Cristiano Ronaldo atakuwepo kwenye kikosi kitakachosafiri kwenda nchini Thailand siku ya Ijumaa kwa ajiri ya kuanza safari yao ya pre-season, lakini Man Utd wamesisitiza kuwa atakuwepo kwenye kikosi kwa msimu ujao.

Cristiano Ronaldo kutokuwasiri klabuni, je ni sehemu ya shinikizo la kutaka kuuzwa au anamatatizo ya kifamilia? ni fumbo ambalo tunasubili majibu kutoka kwake.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa