Cristiano Ronaldo anaripotiwa kuwa sasa anatazamia kuwa atalazimisha uhamisho wake klabuni hapo, kama Juventus watashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Wikiendi iliyopita Juventus waliruhusu kichapo cha bao 3-0 wakiwa nyumbani dhidi ya wapinzani wao wa Serie A wikiendi iliyopita, na wakajikuta wakishuka hadi nafasi ya tano ya msimamo wa ligi, wakati Napoli wakichukua nafasi yao kwenye 4 bora.

Ronaldo anaweza kuikosa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza, kwa miaka 18 kama Juventus ikishindwa kumaliza ligi kwenye nafasi ya nne bora.

Ronaldo Juventus

Taarifa zinasema kuwa, nyota huyu ambaye ana mwaka mmoja ambao bado umesalia kwenye mkataba wake atalazimisha klabu iweze kufanya uhamisho wake kwenda klabu ambayo inashiriki ligi ya mabingwa.

Juventus bado wana mechi dhidi ya Inter, Sassuolo na Bologna kwenye mechi zao tatu za mwisho za Serie A msimu huu, mechi hizi ni muhimu kwao katika jaribio la kurejea kwenye 4 bora ili wafuzu kucheza ligi ya Mabingwa.


 

PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Ronaldo, Cristiano Ronaldo Kulazimisha Uhamisho Juve, Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa