Cristiano Ronaldo Kwenda Barcelona?

Kuna ripoti kuwa klabu ya Juventus inafikiria kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda klabu ya Barcelona na tayari ofa ya klabu hiyo imepelekwa kwa mabingwa hawa wa Laliga.

Taarifa zinasema kuwa klabu ya Juventus inataka kujiondoa kwenye mzigo wa kumlipa Cristiano Ronaldo Mshahara mkubwa.

Hali ya uchumi ya vilabu vingi sasa imedorora kutokana na janga la Corona, Juventus ni moja ya vilabu vinavyotajwa kuathirika pia. Klabu sasa inahitaji kupunguza mzigo wa Euro milioni 28 zinazolipwa kama mshahara wa mwezi kwa Cristiano Ronaldo.

Chanzo kimoja kutoka Italia kinasema kuwa Ronaldo amekuwa mzigo katika kipengele cha malipo kwa Juventus kwa sasa. Hali ngumu ya klabu inawafanya wawe hawana namna zaidi ya kufikiria kumuuza kwenda klabu nyingine ambayo itaweza kumnunua.

Juventus v Genoa CFC - Serie A
Ronaldo

Hata hivyo, karibu kila timu imekumbwa na changamoto ya kiuchumi, Barcelona pia ni miongoni mwa klabu ambazo zimekubwa na changamoto kubwa ya kiuchumi.

Ronaldo mwenyewe hajapatikana akizungumzia hatma yake kwa sasa. Na baada ya kuondoka kwa Maurizio Sarri hatma yake klabuni hapo imeendelea kubaki kuwa na walakini.

Kuna klabu ya kumudu mshahara wa Cristiano Ronaldo kwa sasa? Karibu vilabu vyote vimepata changamoto ya kiuchumi.

Chanzo kimoja kilinukuliwa kikisema “Ofa yake imetolewa kwenda popotea, wakiwemo Barcelona. Lakini, ni kazi sana kuachana na Juventus kwa sasa ukizingatia mshahara mkubwa wanaomlipa. Ni klabu gani ipo tayari kumlipa pesa hiyo?”

Ikiwa Barcelona wataamua kuipokea ofa hii na kuendana na hali waliyokuwa nayo ya kiuchumi, basi huu ndiyo wakati ambao wapinzani wa mda mrefu Lionel Messi na Cristiano Ronaldo watakuwa pamoja.

Hata hivyo, kuna taarifa zingine ambazo zinadai kuwa Ronaldo, ambaye bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake, alikuwa anafikiria kwenda Paris Saint Germain. PSG pia wanatajwa kuwa miongoni mwa klabu zilizopokea ofa ya kumnunua Ronaldo lakini hawajafanyia kazi kwa ukaribu zaidi.


 

Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma Zaidi

 

35 Komentara

    Kambi popote tu nenda cr7 #Meridianbettz

    Jibu

    Asaiv club zote zimeyumba kiuchumi mshahara wa Cr7 ni mrefu atakaa sokoni muda mrefu kdogo

    Jibu

    Usitufokee DEAL swap

    Jibu

    Kwa ali ya sasa himeshuka sana toka mripuko wa hugonjwa wa korona clabu yingi zimeshuka ki uchumi na sijui kama kuna clabu yoyote hitakayoweza kumsajiri Ronaldo

    Jibu

    Hii ni kubwa kuliko na kwa upande wangu ni ngumu kwa mafahari wawili kukaa zizi moja

    Jibu

    Duuh sidhani kama itawezekana maana kama haikai akilini mwangu vile ila ngoja tuuone ukweli utakua wapi ataenda au propaganda za mtandaoni

    Jibu

    Safari njema

    Jibu

    Hi itakuwa kalii Sana Cristian Ronaldo kucheza timu moja Lionel Messi ila ngoja tujionee wenyewe

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Sipati picha huku CR 7 huku Messi hatar sana 👍 nataman kuona hivyo

    Jibu

    Hakuna Klabu inaweza kuwa tayari kununua mchezaji kwa gharama kubwa mwenye umri wa Ronaldo wa miaka 35. Nilishangazwa na mshahara wa Ramsey , ni mkubwa mno#meridianbettz

    Jibu

    Duuu itawezekana kweliii

    Jibu

    Sidhan kama n kwel

    Jibu

    Aiwezekani

    Jibu

    Mmmh hapo mafahari wawili wataweza kukaa zizi moja kwelo itakuaje sasa

    Jibu

    Hii ni ngum sana

    Jibu

    Asanten kwa habari

    Jibu

    Sijui dili likifanikiwa itakuwaje huku Messi huku cr7 kitawaka

    Jibu

    ronaldo abaki apo alipo maana hawezi kufanya kazi na messi uyo watavurugana

    Jibu

    Pale mafahari wawil watapokaa zizi moja

    Jibu

    Mmmh itakuwa ngumu kwa kweli

    Jibu

    Kutokana na pesa nyingi sana anazo lipya cr7 kama PSG watakuwa nazo ni vema zaidi kumchukiwa ila sio rahisi mahasimu wawili kuwa pamoja lazima mmoja wapo aachie ngazi

    Jibu

    Juve wangalie namna ya kufanya ili kuongeza mapato club kwao kumuuza Ronald kwenda bar sio jambo lahisi

    Jibu

    sa itakuaje

    Jibu

    Mmmmh! Mambo magumu!!!

    Jibu

    Duu atalii

    Jibu

    Duu inapendeza sana

    Jibu

    Nataman kuona iyo Messi na Ronaldo timu moja

    Jibu

    Cdhan kama kuna ukwel hapa

    Jibu

    Mmh ngum sana kwa mess kucheza na ronaldo

    Jibu

    Hii ni kubwa kuliko na kwa upande wangu ni ngumu kwa mafahari wawili kukaa zizi moja ?utakuwa ni history tu

    Jibu

    Haaaaaaa Yamewakuta Ila Ronaldo anauzika popote wamuuze tu#Meridianbettz

    Jibu

    Cr7 kazi kazi ila kutakuwa ubaguzi nahisi maana kwa mfumo wa barca pasi zote zipitie kwa messi he ronaldo akienda itakuaje?

    Jibu

    Hii itakua Kali ya dunia cr7 na messi kucheza pamoja duh wapenzi wa PS hua tunashuhudia huko tu.

    Jibu

    Mmmh haiwezekqn

    Jibu

Acha ujumbe