Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo ambacho kinasafiri kwenye tour ya Pre-Season ambacho kinatarajia kusafiri kwenda nchini Thailand na Australia.

Cristiano Ronaldo amewasilisha ombi la kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo, baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja kwenye mkataba wake wa miaka miwili. Mpaka sasa ni Ronaldo tu ambaye hajaripoti klabuni kwa ajiri ya mazoezi ya kujianda na michezo ya Pre-season.

Cristiano Ronaldo, Cristiano Ronaldo Nje Kwenye Kikosi cha Pre-Season, Meridianbet

Cristiano Ronaldo hatasafiri na timu, kwenye kikosi kilichotolewa leo kwa ajiri ya safari ya michezo ya Pre-season, ukiachana na CR7, pia Phil Jones, Brandon Williams, Teden Mengi, Alvaro Fernandez na Shola Shoretire nao hawatasafiri na timu.

Kukosekana kwa Ronaldo kunatoa nafasi kwa kinda Alejandro Garnacho kupata muda wakucheza zaidi, huku Antony Martial na Amad nao watakuwa sehemu ya kikosi hicho baada ya kurudi kutoka kwa mkopo.

Kikosi kizima ambacho kinatarajia kusafiri kwenye michezo ya Pre-season:- De Gea, Lindelof, Bailly, Maguire, Bruno, Martial, Rashford, Malacia, Amad, Fred, Varane, Dalot, Heaton, Shaw, Sancho, Telles, Pellistri, Wan-Bissaka, Bishop, Van de Beek, Elanga, Garner, Tuanzebe, McTominay, Kovar, Laird, Chong, Hannibal, Garnacho, Savage, Iqbal


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa