Mshambulia wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amekusudia kubaki kwenye klabu hiyo hata kama klabu hiyo haitafuzu kucheza mashindano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Ureno kwa mara ya kwanza anarudi kwenye dimba la Old Trafford, na ndani ya miaka 16 aliyotumia nje ya klabu ya Man Utd na kwa mara ya kwanza atamaliza msimu pasipo taji lolote ndani ya miaka 16.
Japokuwa klabu ya Man Utd inasuasua, lakini Cristiano Ronaldo amepanga kubaki kwenye kikosi cha mashetani wekundu kwa msimu ujao, hata kama ikishindwa kufuzu kushiriki mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Man Utd imeondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na klabu ya ATL Madrid kwa ushindi wa goli 0-1, kwenye mchezo wa pili uliochezwa kwenye dimba la Old Trafford, wakati mchezo wa kwanza walitoka sare ya 1-1.
Ushiriki wa Man Utd kwa msimu ujao kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya uko shakani, baada ya kuwa nafasi ya tano kwenye ligi kuu ya Uingereza chini ya klabu ya Arsenal, ambayo inashika nafasi ya nne huku wakiwa na michezo miwili mikononi.
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.