Juventus wanaenda kuumana na Benevento bila staa wao Cristiano Ronaldo.
Wikiendi ya bomba ya soka inafunguliwa na gemu kibao kutoka ligi mbali mbali. Serie A nako kutakuwa kumekucha kukiwa na mechi kadhaa siku ya Jumamosi.

Tarifa zinasema Juve wanatarajia kumpumzisha CR7 katika mechi ya kesho Jumamosi, wakati wakitarajia kurejea kwa Leonardo Bonucci.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports Italia, meneja Andrea Pirlo anataka kuitumia fursa hii kufanya mabadiliko kadhaa kikosini pale anapokaribishwa na mwenyeji wake.

Ronaldo

Ronaldo anakimbizana na Zlatan Ibrahimovic katika nafasi ya ufungaji bora, lakini sasa anaonekana hataweza kufanya mabadiliko yeyote kwenye idadi ya magoli yake wikiendi hii kama anaenda kupumzika.

Wakati Ronaldo akiwa anaenda kupumzika, bila shaka Paulo Dybala au Dejan Kulusevski ataanza pamoja na Alvaro Morata. Daniolo pia anatarajiwa kupumzishwa ikiwa Bonucci ataweza kurejea na kuanza kwenye mechi hii.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

  1. CR7 hajazoea kbs bench na hivi karibuni Pirlo alisema Ronaldo ni sawa na wachezaji wengine ndani ya club hii ni sawa na kusema sio special na CR7 ni brand ya ligi ya Italy kwa sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa