Croatia Mambo Magumu Euro 2024

Timu ya taifa ya Croatia imekua na wakati mgumu kwenye michuano ya Euro 2024 baada ya kushindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo yake miwili ya awali ambayo wamecheza.

Croatia leo wameshuka dimbani kumenyana na timu ya taifa ya Albania kwenye mchezo wa pili wa kundi B ambapo wamelazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Ambapo Croatia sasa watahitajika kuomba washinde mchezo wa mwisho dhidi ya Italy angalau wapate alama nne.

Ikumbukwe mchezo wa kwanza walipoteza kwa mabao matatu kwa bila mbele ya timu ya taifa ya Hispania na leo wanalazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Albania, Hivo mpaka sasa timu hiyo imevuna alama moja tu kwenye michezo miwili ambayo imecheza.croatiaCroatia mshindi wa tatu kombe la dunia mwaka 2022 wameonekana kua na wakati mgumu sana kwenye michuano hii licha ya kua na wachezaji wake bora wote, Huku sasa wakibaki kuomba dua kwenye mchezo wa kesho angalau uishi kwa sare au mmoja apoteze ili wao waendelee kua na nafasi katika mchezo wa mwisho ambao wao pia watatakiwa kushinda dhidi ya Italy.

Acha ujumbe