Crystal Palace Kumchukua Smith Rowe

Klabu ya Crystal Palace wana mpango wa kuhakikisha wanapata saini ya kiungo wa klabu ya Arsenal Emile Smith Rowe ambaye amekua hapati nafasi ya kutosha ndani ya klabu hiyo.

Kiungo Smith Rowe alikua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha Arsenal kwenye misimu mitatu hapo nyuma, Lakini stori ilibadilika kwa mchezaji huyo baada ya kuanza kuandamwa na majeraha ya hapa na pale na kumfanya kupoteza nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha Arsenal.crystal palaceCrystal Palace chini ya kocha Oliver Glasner inamuhitaji kwelikweli mchezaji huyo huku kocha huyo akielezwa ndio amemuhitaji kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza, Palace wametuma ofa kwa klabu ya Arsenal juu ya kiungo huyo wakisubiri kuona ni watapata majibu gani kutoka kwa Washika mitutu wa London.

Klabu ya Fulham ilipeleka ofa kwa Arsenal kumuhitaji Smith Rowe mwanzoni mwa wiki japokua ofa yao ilipigwa chini, Huku Crystal Palace wao wakiwa na matumaini makubwa ya kumpata mchezaji huyo ambaye ni kipenzi cha kocha Oliver Glasner.

Acha ujumbe