Crystal Palace Yamsajili Gallagher Kwa Mkopo.

 

Klabu ya Crystal Palace imekamilisha usajili wa kiungo Conor Gallagher kutoka Chelsea kwa mkopo wa mwaka mmoja.

 

Utakuwa msimu wa pili kwa mkopo katika Ligi ya Premia kwa mchezaji huyo wa miaka 21, ambaye alicheza mechi 32 na kufunga mabao mawili akiwa na West Brom msimu uliopita.

Aliwahi pia kuitumikia Charlton Athletic na Swansea City kwenye maashindano, akicheza michezo 77 ya wakubwa kwa jumla katika miaka miwili iliyopita.

Kiungo huyo anajiunga na timu ya Crystal Palace  inayosimamiwa na nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira, pamoja na Marc Guehi ambaye walikipiga pamoja Chelsea.

Baada ya kurudi kwa msimu huu chini ya Thomas Tuchel na kucheza kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Peterborough United na Bournemouth, mchezaji huyo sasa anaelekea katika viunga vya Selhurst Park.


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe