Cucurella Aingia Rada za Man United

Beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Hispania Marc Cucurella ameingia kwenye rada za klabu ya Manchester United kuelekea kwenye dirisha la usajili kufungwa.

Manchester United wanatajwa kuulizia huduma ya beki Cucurela ambaye haonekani kama chaguo la kwanza ndani ya klabu ya Chelsea na mashetani hao wekundu wanamuhitaji beki huyo kwa mopo na kama watauziwa basi sio kwa gharama kubwa.cucurellaKlabu hiyo inahitaji beki wa kushoto haraka kwasasa kwasababu mabeki wote wa kushoto wamepata majeraha, Hivo wameingia kusokoni kuwinda beki wa kushoto kipindi ambacho Luke Shaw na Malacia wanauguza majeraha yao.

Beki Cucurella yupo kwenye orodha ya juu ya Man United ambaye anaangaliwa kama mbadala mzuri katika kipindi ambacho mabeki wa klabu hiyo wakiwa na majeraha ambayo bado haijajulikana yatapona lini.cucurellaManchester United wamekumbwa na majeraha ya ghafla haswa kwenye upande wao wa kushoto ambao mabeki wake chaguo la kwanza wote wamepata majeraha, Hivo wamelazimika kuingia sokoni kutafuta beki wa kushoto ambapo beki huyo wa Chelsea ndio amekua tageti ya kwanza.

Acha ujumbe