Beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea Marc Cucurella ameweka wazi kua wana furaha kubwa kama wachezaji kutokana na uteuzi wa kocha mpya wa klabu hiyo Enzo Maresca.


Kama ambavyo Cucurella ameonesha upendo na kumpokea kocha huyo kuelekea msimu ujao vivo hivyo wachezaji wengine wanatarajiwa kumpokea kocha huyo, Kwani tayari ndio mwalimu mpya wa klabu hiyo na wanapaswa kumpa ushirikiano ili kuweza kufanya kazi vizuri.