Mshambuliaji wa Atletico Madrid Matheus Cunha ambaye yupo kwa mkopo klabu ya Wolverhampton kwa mkopo inatajwa atasalia klabuni hapo jumla baada ya kumalizika kwa mkopo wake.

Klabu ya Wolverhampton imeamua kumsaini jumla mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil baada ya kumchukua kwa mkopo kwenye majira haya ya baridi mwezi Januari. Mchezaji huyo ambaye mpaka sasa amefanikiw akucheza michezo mitatu kwenye klabu hiyo.CunhaInaelezwa klabu ya Wolves inakaribia kulipa kiasi cha Euro milioni 50 kwa klabu ya Atletico Madrid ili kuweza kupata saini ya kudumu ya mchezaji Matheus Cunha. Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 23 ameonekana kumvutia mwalimu aliyepo klabuni hapo Julien Lopetegui.

Kocha wa klabu ya Wolves Julien Lopetegui inaelezwa ndio amevutiwa na kiwngo cha mshambuliaji Matheus Cunha, Hivo kuhitaji mshambuliaji huyo achukuliwe jumla kutoka klabu ya Atletico Madrid kwasababu anafaa kwenye mradi wake wa siku za mbeleni.CunhaKlabu ya Atletico Madrid imewaachia wachezaji wake kadhaa muhimu kwenye dirisha dogo la mwezi Januari kitu ambacho kimewashangaza wengi, Lakini taarifa zinaeleza tatizo la kiuchumi linaikabili klabu hiyo na ndio sababu ya kuachia baadhi ya wachezaji wake nyota.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa