Beki wa kulia wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Diogo Dalot inaelezwa klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za kumuongezea mkataba beki huyo aendelee kusalia klabuni hapo.

Beki huyo wa pembeni wa Manchester United ambaye alijiunga klabuni hapo mwaka 2018 ukiwa usajili wa kocha mreno Jose Mourinho. Beki huyo amekua hapati nafasi mara kwa mara klabuni hapo kutokana na uwezo wake kutokuwaridhidha makocha waliokuepo klabuni hapo.dalotDalot amefanikiwa kuonesha ubora mkubwa sana tangu kuja kwa kocha mpya ndani ya klabu ya Manchester United msimu huu, Beki huyo amekua kwenye ubora mkubwa mpka kufikia kumshawishi kocha wa klabu hiyo Eric Ten Hag na kufanya kuhitaji aongezewe mkataba.

Klabu ya manchester United ina mpango wa kuingia sokoni kutafuta beki wa kulia ambaye atasaidiana na beki huyo wa kireno kwani wana mpango wa kumuuza beki wa kulia wa timu hiyo Aaron Wan Bissaka kutoka na kutomvutia kocha Ten Hag.dalotDiogo Dalot ambaye kwasasa anaitumikia timu ya taifa ya Ureno kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Klabu ya Manchester United inajiandaa kukaa mezani na beki huyo ili kumuongezea mkataba aendelee kusalia katika viunga vya Old Trafford.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa