Mchezaji wa kimataifa wa Brazili Dani Alves bado anaendelea kucheza soka japo ana umri wa miaka 39 na anatarajia kusafiri na kikosi cha timu hiyo ya taifa kwenye michuano ya kombe la Dunia nchini Qatar.
Ikiwa atasafiri na kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwenyemichuano ya kombe la Dinia, basi atakuwa ni mchezaji mwenye umri mkubwa kutoka taifa hilo kucheza michuano hiyo mikubwa duniani inayotarajia kutimua vumbi mwezi Novemba mwaka huu.
Dani Alves anarekodi ya kuwa mchezaji aliyebeba makombe mengi kuliko mchezaji yoyote duniani kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, sio Lionel Messi, sio Cristiano Ronaldo, wala Pelé ambaye anaweza kumfikia. Na bado anataka kuongeza medali iliyokoseka kwenye kabati lake ambayo ni ya kombe la Dunia tu.
“Hatua muhimu mara zote zimekuwa zikija, sitaweza kuzizuia itakapo fika mwisho, lakini naweza kuendelea kujizuia mwenyewe na hicho ndicho ninachoweza jufanya. Watu wanaangalia umri wangu, lakini hawaishi na mimi. Hawaoni gharama ninazolipa kila siku, jinsi ninavyojitoa na ilikuweza kuwa hivi. Alisema Dani Alves
“Mimi ndio mtengenezaji wa njia yangu, nitaendelea kufanya vitu kwa jinsi niwezavyo, na kama sitaki tena kufanya sitafanya tena, sitafanya na nitakuwa sawa na hilo. Lakini najua kwamba nikiwa uwanjani kucheza, nitacheza.”
Dani Alves ni moja ya wachezaji waliojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazili kinachocheza michezo ya kirafiki, ambapo amecheza kwenye mchezo wa ushindi dhidi ya Japan.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!