Dani Alves beki wa zamani wa klabu ya Fc Barcelona na timu ya taifa ya Brazil amefunguka kuhusu staa wa Manchester United Cristiano Ronaldo.
Beki huyo aleiwahi kua beki bora zaidi wa upande wa kulia duniani ameweza kueleza namna gani anamkubali staa huyo wa klabu ya Manchester United baada ya kusema anamkubali na kumheshimu staa huyo.
Katika mahojiano ambayo amefanya hivi karibuni beki huyu alisema “Nampenda Ronaldo kwasasa hatupo tena kwenye ushindani wa Real madrid dhidi ya Barca,Ambapo kila siku ilionekana huwezi kuzungumza lakini sasa naweza kuzungumza”.
Alves aliongeza kwa kusema “Namheshimu sana hata wakati nilikua nacheza dhidi nilimpa heshima kubwa”.
Nyota huyo wa kibrazil inakua sio mara ya kwanza kumuongelea staa huyo kwani pia ameshawahi kueleza ni mchezaji gani imewahi kua ngumu zaidi kukabiliana nae bila kusita alimtaja staa huyo wa kireno.
Dani ameonesha uungwana baada ya kutoa heshima kwa Ronaldo na kitendo hicho kimeleta mapokeo tofauti kwani kuna baadhi wameona ni kitendo cha kiungwana lakini wengine wakidai ni msaliti baada ya kuachwa na klabu ya Barcelona mwanzoni mwa msimu huu.