Dani Olmo Aingia Rada za Man City

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Rb Leipzig ambaye anakipiga timu ya taifa ya Hispania kwasasa kwenye michuano ya Euro 2024 Dani Olmo ameingia kwenye rada za klabu ya Manchester City.

Manchester City inaelezwa kua klabu ya karibu zaidi inayofukuzia saini ya Dani Olmo ambaye amekua akionesha ubora na mkubwa ndani ya kikosi cha Rb Leipzig, Lakini pia moja ya wachezaji bora wa kikosi cha Hispania ambao wamefanya kazi kubwa mpaka sasa timu hiyo kufika fainali ya Euro 2024.dani olmoKiungo huyo amekua na misimu bora sana ndani ya klabu ya Rb Leipzig lakini timu kubwa mbalimbali ulaya hazikua zimeonesha kumuhitaji mpaka wapenzi wa soka kumuona kama mchezaji asie na bahati, Lakini awamu hii klabu ya Man City imeelezwa kuulizia huduma yake.

Kiasi ambacho kinapaswa kulipwa kumpata mchezaji huyo ni Euro milioni 60 kwa klabu ambayo itaweza kulipa kiasi hicho basi inaweza kumpata Dani Olmo, Klabu ya Man City inaelezwa kua tayari kutoa kiasi hicho japokua inaweza kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa klabu ya Chelsea.

Acha ujumbe