Kiungo wa kimataifa wa Hispania ambaye alikua anakipiga klabu ya Rb Leipzig Dani Olmo amefanikiwa kujiunga klabu ya Barcelona kwa mkataba wa miaka sita ambao utamuweka klabuni hapo mpaka 2030.
Dani Olmo amekamilisha usajili wake wa kujiunga na miamba ya soka nchini Hispania baada ya mvutano wa wiki kadhaa baina ya klabu ya Barcelona dhidi ya Rb Leipzig, Lakini hatimae vilabu hivo vimefikia makubaliano na kiungo huyo mfungaji bora wa miachuano ya Euro 2024 atacheza Barca msimu ujao.Barcelona wametoa kaisi cha Euro milioni 55 na nyongeza ya Euro milioni 7 ambayo itatoka siku za mbeleni kutokana na vipengele walivyoekeana hivo jumla ya pesa iliyotumika kumpata kiungo huyo ni Euro milioni 62, Licha ya Barca kua kwenye kipindi kigumu kiuchumi lakini wamepambana kuhakikisha wanapata ya kiungo huyo.
Kiungo Dani Olmo ambaye amewahi kupita akademi ya klabu ya Barcelona ndio kwa kiwnago kikubwa amerahisisha kukamilika kwa dili hili, Kwani kiungo huyo alikua ameonesha nia ya wazi ya kutaka kujiunga na klabu ya Barcelona klabu ambayo ilimlea na kukuza kisoka miaka mingi iliyopita.