Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Danny Ings amefanikiwa kujiunga na klabu ya West Ham kwa mkataba wa kudumu akitokea klabu ya Aston Villa katika dirisha hili la mwezi Januari kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 12.
Klabu ya soka ya Aston Villa imekubaliana na West Ham kumnunua mshambuliaji Danny Ings ambae amekua na wakati mzuri ndani ya klabu hiyo. Mshambuliaji huyo sasa ni rasmi atakua mchezaji wa West Ham akienda kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo baada ya kukamilika kwa dili hilo ameonesha kufurahia dili na kusema “Nina furaha sana kujiunga na klabu hii, Ni muhimu nitulie haraka iwezekanavyo ili niweze kufanya mambo muhimu uwanjani kwa kalbu hii ya West Ham” Aliyasema hayo mshambuliaji huyo.
Mshambuliaji huyo anakwenda kuungana na washambuliaji kama Giancluca Scamacca, Antonio pamoja na Said Benrahma na kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu ya West Ham. Huku mchezaji huyo ikielezw ni pendekezo la moja kwa moja la kocha wa timu hiyo David Moyes.
Mshambuliaji Danny Ings anaingia kwenye rekodi kua miongoni mwa wachezaji waliocheza kwenye timu nyingi ndani ya ligi kuu ya Uingereza akiwa ameshacheza timu sita mpaka sasa. Mchezaji huyo amewahi kupita vilabu vya Bournamouth, Burnley, Liverpool, Southampton, Aston Vila, pamoja na West Ham ambayo anaitumikia kwasasa.


