Beki wa RB Leipzig na timu ya Taifa ya Ufaransa – Dayot Upamecano anaendelea kuviteka vichwa vya habari ulimwenguni kuhusu hatma yake kwenye ulimwengu wa soka.
Ni nani ataipata lulu hii ambayo inaonekana kama ndio tiba ya timu nyingi barani Ulaya zinazotaabika kwenye safu zao za ulinzi?
Akiwa na umri wa miaka 22 pekee, Dayot Upamecano anahusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali. Liverpool, Manchester United, Bayern Munich na Real Madrid ni miongoni mwa timu zinazoiwinda saini ya beki huyu mahiri.
Mkataba wa Upamecano ndani ya Leipzig unakipengele cha kuruhusu mchezaji huyo kuuzwa kwa dau la pauni milioni 40 mwishoni mwa msimu huu. Japokuwa, taarifa zimeripoti uwezekano wa beki huyo kuuzwa mapema mwezi Januari kama tu, timu itafikia dau lililopo kwenye mkataba wake.
Inasemekana Bayern Munich wamejitoa kwenye mbio za kuisaka saini ya Dayot Upamecano kutokana na sababu za kiuchumi. Licha ya kwamba Bayern huenda ikawakosa mabeki wake wawili – David Alaba na Jerome Boateng mwishoni mwa msimu kufuatia kuisha kwa mikataba yao, bado dau la Upamecano ni kubwa kwa Bayern kujitosa sokoni.
Kwa upande wa Madrid, inaaminika kocha – Zinedine Zidane anamtizama Upamecano kama mrithi sahihi wa nahodha wa kikosi hicho – Sergio Ramos. Ikiwa mpaka sasa hatma ya Ramos haijajulikana, huenda Madrid wakajitosa kuingia sokoni mapema na kuitafuta saini ya Upamecano.
Nchini uingereza kuna vita ya aina yake linapokuja suala la usajili. Liverpool na Manchester United ni mahasimu wa Ligi Soka nchini Uingereza. Kwa miaka mingi wamekuwa hawauziani wachezaji kutokana na uhasimu wao. Hapa takayempata Upamecano atakuwa ameshinda vita kubwa.
Liverpool inataabika na idadi kubwa ya majeruhi kwenye kikosi hicho. Mpaka sasa, wachezaji wote wa safu ya ulinzi wanaocheza kikosi cha kwanza ni majeruhi na watakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu. Hili ni pigo kwa Jurgen Klopp na atalazimika kuingia sokoni mapema iwezekanavyo.
Je, Klopp atajitosa kumsajili Dayot Upamecano kwa dau lililowekwa au wataamua kuwatumia wachezaji wao wenye uwezo wa kuziba mapengo kwenye safu ya ulinzi? Hili bado ni swali ambalo majibu yake pengine yatapatikana kuanzia Januari 1, 2021.
Ole Gunnar Solskjaer bado hajatibu tatizo kwenye safu yake ya ulinzi licha ya kuwasajili Aaron Wan-Bissaka, Harry Maguire na Alex Telles kama walinzi wa miamba hiyo ya Old Trafford.
United wanahitaji beki wa kati mwenye kasi ya kuanzisha na kuzuia mashambulizi na atakayeweza kucheza vizuri na Harry Maguire ambaye hana kasi kubwa katika uchezaji wake. Dayot Upamecano alitajwa sana kama mchezaji anayehitajika zaidi kwenye kikosi cha United lakini usajili wake haukuwezekana katika dirisha la usajili lililopita. Je, Januari United wataweka pesa mezani na kumchukua mchezaji wanayemuwinda kwa muda mrefu?
Uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi na kulinda timu yake pamoja na kufunga magoli, ni kati ya vitu vikubwa alivyonavyo Upamecano. Umri wake ni mdogo na hivyo ni faida kwa timu yeyote itakofanikiwa kuipata huduma yake.
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.
Angelina
Goodupdate
Sauda
Upamecano ana rekodi nzuri sana
Devotha
Yupo vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Safii sana
Samira
Rekodi yake nzuri ndio inapelekea kuwindwa na wengi na yoyote atakaefanikiwa kumpata anatakua msaada mkubwa hasa kwa timu ambazo bado hazifanyi vizuri
Sadick
Dayot Upamecano alicheza vizuri mno mechi ya LEIPZIG dhidi ya PSG hilo lilimuweka kwenye rada za Klabu duniani
Caroline
Dayot yupo vizuri
Ester jackson
Bora aende real Madrid akawike vizuri
Rahma
Dayot nimemuelewa
Fatina mfingi
Nice
Nasra
Safi
Saupha mohamed
Good
Fatuma kasomo
Yupo vizur
aisha
Anajua ndio maana wanamgombea
Sabrina
Dayot anajua
felister
yupo vizuriii
Janeflora malisa
Safi
David Pere
Inasemekana Bayern Munich wamejitoa kwenye mbio za kuisaka saini ya Dayot Upamecano kutokana na sababu za kiuchumi. Licha ya kwamba Bayern huenda ikawakosa mabeki wake wawili – David Alaba na Jerome Boateng mwishoni mwa msimu kufuatia kuisha kwa mikataba yao, bado dau la Upamecano ni
Issa
Upamecano lulu iatakasumbua kwenye soka
magdalena
kijana yupo vizuri ndo maana analiliwa na wengi
Ernest
Ni wakati wake sasa Dayot Upamecano kulamba deal nono
zeiyana
Subili tuangalie mtazamo wake mwenyew clabu hipi hataenda kuichezea
Hopemwaikuka
Dodo limekwiva kaz kwao walaj
Povel
Nice update