Kevin de Bruyne alipuuza pendekezo lolote la masuala ndani ya timu na kushuka kwa kiwango kwa mshambuliaji nyota wa Manchester City Erling Haaland.
Haaland amekuwa katika hali ya kuvutia katika kampeni yake ya kwanza na klabu, akifunga mabao 34 katika mechi zote kwenye mashindano yote.
Hata hivyo, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Norway amefunga mabao matatu pekee katika mechi tisa zilizopita, na kusababisha mapendekezo kuwa kiwango chake cha uchezaji kimeshuka.
De Bruyne haoni hivyo ingawa, akieleza kuwa timu zimejiandaa zaidi kukabiliana naye sasa kuliko ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu.
Mchezaji juyo ameongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa; “Nadhani ni kila kitu lakini sijisikii ni tofauti na hapo mwanzo, labda  watu wanamsubiri zaidi mbio zake, huwa kuna sehemu ya kwanza ya msimu halafu sehemu ya pili, sehemu ya pili, nahisi timu zimejipanga zaidi, zinacheza kwa zaidi kutoka pande zote, kwa hivyo watu wamejitayarisha zaidi kwa kila maana ya njia.”
De Bruyne anasema kuwa waliona mchezo wa Crystal Palace, angeweza kufunga mabao mawili na kuna suala la wazi watu huwa wanamtarajia kufunga mabao mawili au matatu lakini wastani wake ni bao kwa mchezo na inaonekana ni sawa kwake.
Anakazia kuwa hadhani kama kuna tatizo na kitu chochote kutoka kwa timu au kwa Erling. Anajua watu watahukumu jinsi wanavyocheza na labda wakati mwingine wanacheza chapa bora ya kandanda katika michezo tofauti au miaka mingine lakini hiyo hufanyika.