De Gea Atimka Rasmi Man United

Aliyekua golikipa wa klabu ya Manchester United David De Gea ametangaza kuachana na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa kipindi kirefu na anaondoka kama mchezaji huru.

De Gea ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2011 akiwa mpaka sasa ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 12, Leo kupitia mitandao ya kijamii ameandika kua leo ndio mwisho wa utumishi wake kama mchezaji wa klabu hiyo.Golikipa huyo raia wa kimataifa wa Hispania ameondoka klabuni hapo kwa taarifa za kushtukiza kwani golikipa huyo ilitaarifiwa kua yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo kwa kipindi kirefu lakini haikua hivo.

Golikipa De Gea anaondoka ndani ya Man United akiwa amefanikiwa kwa kiwango kikubwa, Kwani ametwaa taji la ligi kuu ya Uingereza,FA, Carabao,Europa, pamoja na Ngao ya jamii hii inaonesha kua golikipa huyo amefanikiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya timu hiyo.de geaDe Gea ambaye alikua golikipa aliechukua glovu ya dhahabu msimu uliomalizka baada ya kumaliza michezo 15 bila kuruhusu bao msimu ulimalizika, Hivo inaonesha kua golikipa huyo anaondoka kwenye timu hiyo akiwa bado mwenye ubora wa hali ya juu.

Acha ujumbe