De Gea Kinara wa United Mara 3 Mfululizo.

Ni dhahiri kuwa, David De Gea ndiye anayeibeba Manchester United mabegani mwake msimu huu. Ubora wake golini ni msaada tosha.

De Gea amekuwa muhimili imara kwenye goli la Man United msimu huu. Ama hakika, michomo anayookoa, pengine ingezamisha zaidi jahazi la United mpaka sasa msimu huu.

Mwezi Januari ameondoka na tuzo nyingine ya mchezaji bora wa mwezi baada ya kufanya hivyo mwezi Novemba na Disemba.

De Gea

Hii inakua ni mara ya 3 mfululizo kwa De Gea kutwaa tuzo hiyo msimu huu. Kwa mwezi Januari, David ameitumikia United kwenye michezo 5 akiwa hajaruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye michezo 2.

Wastani wa 67% ya kura zilizopigwa na mashabiki wa United zilikwenda kwa David huku Scot McTominay (12%), Bruno Fernandes (11%) na Anthony Elanga (10%) wakikamilisha orodha ya wachezaji waliokuwa wanawania tuzo hiyo.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe