De Gea Kuondoka Man United

Golikipa wa klabu ya Manchester United David De Gea ana uwezekano mkubwa wa kuondoka ndani ya klabu hiyo katika majira haya ya joto baada ya kuitumikia kwa miaka kumi na mbili.

Katika hali ya kushtua golikipa De Gea hajaonekana katika orodha ya majina ya wachezaji wataokuwepo kwenye klabu ya Man United msimu ujao, Hii imeonesha dalili kubwa kua golikipa huyo hatakuepo kwenye viunga vya Old Trafford msimu ujao.de geaKlabu ya Manchester United inaelezwa ipo kwenye mpango wa kutafuta golikipa mwingine sokoni ili kuweza kuziba nafasi ya golikipa huyo alietumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa huku magolikipa kama Andre Onana,Diogo Costa, na Jordan Pickford wakitajwa kumrithi.

David De Gea anatajwa kufanya mazungumzo na klabu ya Al-Hilal kutoka nchini Saudia Arabia ili kuweza kujiunga nayo, Klabu ya Man United ilikua inafanya mazungumzo na kipa huyo kwa muda mrefu lakini wameshindwa kufikia muafaka kwani kipa huyo aligoma kupunguza mshahara wake.de geaGolikipa David De Gea anaondoka ndani ya timu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 12 na kwa mafanikio makubwa huku akibeba kila taji ndani ya klabu hiyo kasoro taji la ligi ya mabingwa ulaya, Hivo Mhispaniola huyo atabaki kukumbukwa na mashabiki wa klabu hiyo gwiji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.