De la Fuente Akemea Tabia ya Argentina

Kocha wa Spain, Luis de la Fuente, ametoa kauli kali dhidi ya wachezaji wa Argentina kufuatia vurugu zilizotokea baada ya fainali ya Kombe la Dunia 2026. Hispania walitwaa ubingwa kwa mara ya pili katika historia yao kwa ushindi wa 1-0 baada ya muda wa nyongeza dhidi ya Argentina kwenye MetLife Stadium, lakini sherehe ziligeuka vurugu.

De la Fuente Akemea Tabia ya Argentina

De la Fuente alisema kupitia televisheni ya Hispania, “Kilichotokea baada ya mechi hakiwezi kukubalika kwa hali yoyote. Tulichokiona hakivumiliki na hakikubaliki. Wachezaji wa kiwango hiki, wakiongozwa na kocha mkubwa, lazima walihisi vibaya walipoona matukio hayo. Hizi ni taswira zisizostahili soka.”

Baada ya mchezo huo wa fainali, vurugu ziliibuka pale Leandro Paredes alipotumia nguvu na kufanya makabiliano ya moja kwa moja na wachezaji wa Hispania hasa hasa Gavi na Eric Garcia. Nahuel Molina alimpiga Rodri. Vilevile, Fabian Ayala, msaidizi wa Lionel Scaloni, anatuhumiwa kumshambulia Dani Olmo.

De la Fuente Akemea Tabia ya Argentina

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha wa La Roja aliwasifu wachezaji wake kwa kutulia na kuonyesha ustaarabu licha ya uchokozi huo. “Ningependa kupongeza tabia ya wachezaji wetu kwa namna walivyodhibiti hali na kuonyesha sportsmanship hadi mwisho,” alisema.

De la Fuente Akemea Tabia ya Argentina

FIFA imefungua uchunguzi rasmi ili kubaini wahusika na kutoa adhabu stahiki. Tukio hili limeibua mjadala mkubwa kuhusu nidhamu na heshima katika soka la kimataifa, hasa kwa wachezaji wa kiwango cha juu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.