De Ligt na Man United ni Suala la Muda

Beki wa kimataifa wa Uholanzi Mathijjs De Ligt na klabu ya Bayern Munich inaelezwa yupo tayari kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha hili kubwa msimu huu.

Beki Mathijjs De Ligt inaelezwa yuko kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na klabu ya Man United na ameonesha yupo tayari kukipiga ndani ya klabu hiyo msimu ujao licha ya klabu hiyo kutoshiriki ligi ya mabingwa ulaya msimu wa 2024/25.de ligtBeki huyo wa zamani wa klabu ya Ajax taarifa zinaeleza yeye pamoja na wakala wake wameshakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Man United, Hivo kinachosubiriwa zaidi ni mazungumzo baina ya klabu ya Man United dhidi ya Bayern Munich ili kupata saini ya beki huyo.

Beki Mathijjs De Ligt amevutiwa na mpango wa mbele waliokua na viongozi wa klabu ya Man United, Lakini mchezaji huyo anavutiwa kujiunga tena kocha wake wa zamani ndani ya klabu ya Ajax ambaye alimpatia nafasi ndani ya kikosi cha Ajax Erik Ten Hag ambaye ni kocha wa Man United kwasasa.

Acha ujumbe