Kocha wa klabu ya Brighton Hove and Albion Roberto de Zerbi amesema kiungo wa klabu hiyo Moises Caicedo ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka mmiliki wa klabu atakapobadilisha mawazo.
Kocha De Zerbi anasema mpka sasa mpango ni kuendelea kubaki na Caicedo na hajui ambacho kitatokea mbeleni, Lakini ameweka wazi kama itatokea mchezaji huyo ataondoka watahitaji kutafuta mchezaji sahihi wa kuziba nafasi yake.Moises Caicedo amekua akiwindwa na klabu ya Chelsea tangu dirisha hili lifunguliwe, Lakini klabu ya Brighton bado haijakubali oa yeyote kutoka klabu ya Chelsea na kocha wa klabu hiyo amebainisha bado wana mpango na mchezaji huyo.
Kocha De Zerbi aliongeza wanatakiwa kuziba nafasi yake kwa kupata mchezaji mwenye ubora kwakua msimu ujao wanacheza michuano ya Uefa Europa League michuano ambayo Chelsea hawashiriki watu wakitafsiri kama kijembe kocha huyo amekitupa kwa Chelsea.Taarifa zinaeleza kiungo Moises Caicedo ameshamalizana na klabu ya Chelsea kwenye maslahi binafsi, huku kinachosubiriwa ni ofa ya klabu ya Chelsea kukubaliwa na klabu ya Brighton ili kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Ecuador.