De Zerbi Kutimka Brighton

Kocha wa klabu ya Brighton Hove and Albion raia wa kimataifa wa Italia Roberto De Zerbi ameweka wazi hana mpango wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa msimu ujao baada ya kukaa klabuni hapo kwa misimu miwili.

De Zerbi amesema tayari ameshaamua kua hataongeza mkataba mpya ndani ya Brighton japokua ametoa nafasi bado, Kwani amesema ataongea na mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Tony Bloom.de zerbiKocha huyo ameonesha wazi kua hana mpango wa kuendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo kwa msimu mwingine ujao, Hii inatokana na kauli ambazo amekua akizitoa hivi karibuni na hii ikionesha huenda hajavutiwa na mkakati wa mbeleni wa klabu hiyo.

Taarifa zinaeleza kua sababu nyingine inayomfanya kocha huyo kutaka kutimka klabuni hapo ni pamoja na kutakiwa na vilabu vikubwa barani ulaya ambavyo mwishoni mwa msimu vitaachana na makocha wake.de zerbiDe Zerbi yupo kwenye orodha ya vilabu kama Bayern Munich, Barcelona, na Liverpool pia vilabu ambavyo msimu huu wataachana na makocha wao, Huku kocha huyo akipigiwa chapuo ya kuchukua kibarua kati ya timu hizo kubwa tatu barani ulaya.

Acha ujumbe