Declan Rice kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza ameahidi mabadiliko kwenye kikosi hicho ambacho kimekua na mfululizo wa matokea mabaya katika siku za karibuni.

Kiungo huyo anayekipiga katika klabu ya West ham ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kupokea kipigo cha bao moja kwa bila dhidi ya Italia katika mchezo uliopigwa katika dimba la San Siro usiku wa kuamkia leo.

Zikiwa zimebakia siku 56 kuelekea fainali za kombe la dunia nchini Qatar kiungo huyo ameahidi maboresho ndani ya kikosi hicho.

declan Rice“Ni wazi inakatisha tamaa, Kwasababu kila michuano tunayokwenda kushiriki tunahitaji kushinda” katika ligi ya mataifa usiku huu tumeshuka viwango ila sidha kama kila kitu kilikua kibaya usiku huu”

“Tutakua sawa tumekua na kiwango kizuri usiku wa leo kuliko tulivyoona kwenye majira ya joto,Sio kwamba hatutengenezi nafasi. “Naona kwenye mazoezi.Kuna mambo mazuri ya kufurahisha yanakuja niamini”alisema Rice.

Kiungo huyo anaamini kuna mambo madogo wanayafanyia kazi na watarudi kwenye ubora wao kuelekea kwenye michuano ya kombe la dunia mwezi wa 11 mwaka huu nchini Qatar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa