Declan Rice  kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya West Ham inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza anamuona staa mwenzake wa taifa hilo Jude Bellingham kama nyota atakayefanya makubwa kwa taifa hilo.

Rice amedai Jude ndo kijana wa miaka 19 mwenye kipaji zaidi kuwahi kumshuhudia yeye,licha ya Uingereza kushuka daraja mwishoni mwa wiki iliyopita ila haikumfanya Declan Rice kumsifu kiungo huyo mwenzake anyekipiga katika klabu ya Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani.

declan riceKatika mchezo wa jumatatu katika mchezo waliocheza dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani uliomalizika kwa suluhu ya magoli matatu kwa matatu nyota Jude Bellingham kumaliza kama mchezaji bora wa mchezo baada ya kucheza kwa kiwango bora kabisa katika mchezo huo.

Declan Rice anaamini nyota huyo ana uwezo wa hali juu pande zote ni wa kipekee kwa mtu wa rika lake aliliambia gazeti la The Mirror: “Sidhani kama nimeona mtu mwenye uwezo wake katika umri wa miaka 19”.

“Nimeangalia vijana wengi wa miaka 19. nchini na duniani kote sijaona kijana ambae amekamilika kila idara kama yeye nafikiri yeye ana hilo”.

declan rice“Ana miaka 19 lakini anaonekana kama ana miaka 28. ni kijana mdogo lakini anacheza kama mwanaume,anafikiri kama mwanaume na anaonesha utu na tabia.

Declan ameeleza mambo mengi sana kumhusu staa mwenzake huyo katika timu ya taifa ya Uingereza ila kubwa zaidi anamuona kama nembo ijayo ya taifa hilo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa