Anatajwa kama nahodha ajaye kwenye kikosi cha West Ham United, mrithi sahihi wa Mark Noble. Declan Rice anamaamuzi ya kufanya mwishoni mwa msimu huu.

Kwa misimu takribani mitatu, Declan Rice amekuwa kwenye kiwango bora kwenye safu ya kiungo, sio akiwa West Ham United tu, hata akiwa na timu ya Taifa ya Uingereza, Rice ni mchezaji muhimu kwenye kikosi.

Uwezo wake wa kutawala katikati mwa uwanja, kukaba na kushambulia wapinzani, uongozi ndani ya uwanja n.k ni sifa muhimu za Rice. Hakika, Chelsea walifanya kosa kumuachia mchezaji huyu angali akiwa bado ni kijana mdogo.

Stamford Bridge ilimtupa nje, London Stadium wakampokea na kumkuza kuwa hivi alivyo sasa hivi. Ni lulu ya The Hammers. The Blues watapaswa kumwaga pesa nyingi ili kumrudisha darajani.

Japokuwa kocha wake amekua akisisitiza Declan Rice hatouzwa kwa pesa ndogo, idadi ya timu zinazomuwinda inaendelea kupungua maradufu, imebaki Manchester United pekee.

Declan Rice, Declan Rice Kuamua Hatma Yake., Meridianbet

Chelsea wanakazi ya kusuka upya idara yao ya ulinzi, Man City watawekeza kwenye idara ya ushambuliaji na beki wa kushoto, Liverpool watawekeza kwenye safu ya kiungo lakini, watasajili mchezaji mwenye gharama nafuu sokoni. Arsenal na Spurs hawana uwezo kabisa wa kuingia kwenye vuguvugu hili kwa misingi ya kiuchumi.

United ndio timu pekee inayoweza kusajili wachezaji wa gharama kubwa pamoja na kulipa mishahara mikubwa. Naam, Manchester United ni klabu kubwa duniani, hili lisisahaulike. Wanamifuko mirefu, wapo kundi moja na Real Madrid kama miamba ya soka la Ulaya.

Japokuwa United hii sio ile ya miaka ya nyuma iliyokuwa inawavutia wachezaji wa kila namna, bado wananguvu sokoni. Declan Rice ataamua, kwenda United msimu huu ukiisha au kubaki London Stadium akisubiri nafasi nyingine kama itatokea kwa vilabu vingine?

West Ham ni mashahidi wa maisha ya soka kwa wachezaji. Lampard, Joe Cole, Carrick, Ince, Ferdinand wote walitoka klabuni hapo na kwenda kufanikiwa kwenye vilabu vingine vikubwa nchini Uingereza.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa