Nahodha wa Watford, Troy Deeney amesema hatarejea mazoezini kwasababu anaohofia afya ya familia yake kipindi hiki cha Corona.
Vilabu vya Premier League vimeanza mazoezi Jumanne ya bila kugusana.
Deeney hataki kumuweka mtoto wake mwenye matatizo ya kupumua kwenye hatari zaidi.
“Tunatakiwa kureja wiki hii, Nimesema siwezi kwenda,” Deeney, 31, alisema.
Watford hawataanza mazoezi Jumanne na inaeleweka klabu haina tatizo na maelezo ya Deeney.
Deeney ameongeza: “Ni mtu mmoja tu akiambukizwa kwenye kundi wote mnaweza kupata, sitaku kupeleka nyumbani..
“Mwanangu ana miezi mitano tu, ana matatizo ya kupumua, hivyo sitaki kurudi nyumbani kumuweka kwenye hatari.”
Last Wednesday, Deeney alikuwa kwenye kikao cha Premier League, na manahodha wa timu nyingine na wataalamu wa afya.
Alisema: “Taizo langu lilikuwa kwenye kikao niliuliza maswali mepesi.
“Kwa watu weusi, Asia na watu waliochanganya mataifa, wana hatari mara nne zaidi kupata maambukizi – je kuna kitu kingine cha ziada, kama mifimu ya kuona changamoto za moyo na mapafu kuona kama watu wanamatatizo hayo? Hapana. Sawa nadhani tufikiria na hilo pia.
“Siwezi kunyoa hadi kati ya Julai lakini naweza kuingia kwenye boksi na watu 19 kuruka kichwa na hakuna wakujibu swali, sio kwamba hawakutaka, lakini hakuwa na taarifa.
“Kwa hiyo nikasema kama hamna taarifa, kwanini nijiweke hatarini?”
Christopher
Vizuri kwake na familia yake maana ameonyesha msimamo
Povel liwongolo
Ni habar mbaya sana kwa wapenz wa Watford kwa mchezaj wao kugoma kwenda kuanza mazoez na wenzak thanks meridian kwa update
mwakalosi
Huyu hayuko tayari kurudi uwanjani kwa sasa
Tahiya
Izo ni habari mbya kwa timu
Evaluziga
Hayupo tayari kuludi uwanjani kwa sasa
David pere
Anajiamini hata bila mazoezi anaweza kukipiga
Tatu
Sio habari nzuri kwa wapenzi wa mpira
Rehema Dickson
Ni vizuri kwake kaonesha msimamo wake na wao watajua wafanye nn ili kumuweka sawa
Emmy cleopa
Ahsante meridian kea taarifa
Ester jackson
Ni vizuri kwake mana anaonyesha anawajali sana familia yake hivyo wanatakiwa kuangalia jambo la msingi la kiafya kabla hajakutana na familia yake akiwa anatoka mazoezini
Antony Luseno
Ana sababu kwa hiyo kilabu yake yapasa iheshimu maamuzi yake
Zeiyana iddi
Deeney uwo ni uwoga..!kwani hao wachezaji wenzako awana family ugonjwa upo huu inatakiwa tukubaliane na ali
Gabriel
Mtata huyo
winfrida
troy upo sawa ni bora kujikinga na kuwakinga ndugu zako kwan corona bado ipo
Genia skaluzwe
Hizo ni habari mbaya kwa mashabiki wa mpira
aisha
Duuh hizo sio habari nzuri kwa wachezaji wenzake maana umoja ni guvu
Neema juma
Ila kwa ajili ya usalama wake nafamilia yake. Hali ikikaa sawa atarudi tu.
Mwajuma
Nijambo jema kujali familiya kwanza
Theonestina
Achukuwe tahadhali tu
Mwanahamisi
Hizo ni habari mbaya kwa wachezaji
Hamidu
Jambo Zuri kujali familia yake.mengine baadaye .asnte meridianbettz kwa habari nzuri za michezo
Khadija
huyo ayuko tayali na ndio maana akawagomea#meridianbettz
frank patrick
Ni taarifa mbaya kwa team lakini ni maamuzi sahihi kwa mchezaji kulingana na sababu zake husika
Magdalena
Mazoezi ni muhimu kwa afya ni vyema akarejea mazoezini #meridianbet
Hidaya Mohammed
Kinga ni bora kuliko tiba
Isaya massawe
Huyu ataki kazi
Juliana
Jaman pole yake,but asihofie sana
Ernest
Kama Professional player hii sio picha nzuri kwani angeweza kujitenga na familia yake kwa kipindi hiki kifupi kwa ajili ya kumalizia ligi alafu mambo mengine yangefuata baadae.
Samira
Anaonyesha kuwavunja moyo wenzake walio tayari kurudi uwanjani
Furahav
Acha uvivu fanya mazoezi.
Mariam mtandama
Duuuh
Salma
Mtovu wa nidhamu
Theckla
Hayo ni maamuzi yake yaheshimiwe
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuru kwake na kwafamilia yake kuonesha msimamo
Samiah
Hana nidhamu huyo
Agness
Asante meridianbet kwa habary mzur
Mwanaidi
Kama mchezaji mahiri hajafanya fair
Ally mohamedi ally
Habar mbaya sna hii