Dejan Kulusevski Kuwapambanisha Spurs na Arsenal

Arsenal na Tottenham Hotspur wanaripotiwa kugombania saini ya mshambuliaji wa Juventus Dejan Kulusevski katika dirisha dogo la usajili la majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo mwenye miaka 21 amecheza mechi 17 na Juventus, kwenye kampeni za 2021-22 lakini ameanza mara mbili pekee kwenye mechi za Serie A, mechi 15 za ugenini msimu huu akitokea benchi.

Hivi majuzi kumekuwa na taarifa kwamba Juventus iko tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi ili kuongeza bajeti yao, huku ofa ya €35m (£29.4m) ikitajwa kuwa mezani.

Dejan Kulusevski
Dejan Kulusevski

Kwa mujibu wa Calciomercato, Arsenal na Tottenham wote wana nia ya kumleta mshambuliaji huyo kwenye Premier League na wanaweza kupambania saini yake mwaka ujao.

Kulusevski, ambaye ana uwezo wa kucheza katika nafasi mbalimbali za mbele, ameona nyavu mara nane na kusajili pasi nane za mabao katika mechi 64 alizoichezea Juventus kwenye mashindano yote.

Vilabu vingi vya Ulaya vinaaminika kutaka kumsajili Msweden huyo, lakini ripoti ya hivi majuzi ilidai kwamba kuhamia Ligi ya Premia ndiyo kuna uwezekano mkubwa zaidi.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe