Dembele Alitamani Kuwa Kama Fernando Torres

Mshambuliaji mpya wa Atletico Madrid, Moussa Dembele anasema kuwa Fernando Torres alikuwa ni alama yake tangia alipokuwa mtoto.

Dembele anatarajiwa kuwa atakuwa mrithi wa nafasi ya Diego Costa ambaye amesitisha mkataba wake mwezi uliopita, mshambuliaji huyu mbya anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya Atleti.

Dembele amefunga alifunga jumla ya magoli 44 kwa misimu yake miwili alipokuwa na Lyon, ambao alijiunga nao 2018 akitokea Celtic. Msimu huu haujawa mzuri sana kwake akiwa ameona nyavu mara moja tu kwa mechi zake 16 alizocheza kwenye Ligue 1.

Rasmi: Moussa Dembele Ajiunga na Atletico Madrid

Dembele ameelezea kuwa mpango wake yeye kwenye klabu yake mpya ni kufunga magoli, kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yake, lakini amesisitiza kuwa legendari wa Atletico Fernando Torres ndiye aliyekuwa akimvutia tangia alipokuwa mtoto.

“Kimsingi, mimi ni straika na ninapenda kufunga magoli. Hiyo ndiyo kazi yangu. Napenda kutengeneza nafasi, kupokea mipira na kufunga magoli. Ni mchezaji mzuri mwenye mbinu. Ninasubiri kwa hamu kuanza kucheza hapa, Nilipokuwa mtoto, Fernando Torres ndiye niliyempenda, alikuwa ni mfano wangu wa kuigwa, hivyo nina furaha kuwa hapa.”

Atletico kwa sasa ni vinara wa LaLiga wakiwa na pointi 41 katika mechi zao 16 walizocheza msimu huu. Wana pointi 4 mbele ya wapinzani wao wa karibu huku wakiwa na gemu 2 mkononi.


MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5

Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!

INGIA MCHEZONI

 

9 Komentara

    Dembele anajua sana

    Jibu

    Dembele yupo vizuri sana

    Jibu

    Huko vzur

    Jibu

    Dembele Yuko vizuli sana

    Jibu

    Dembele apambane Sana atakuwa tu kama yeye

    Jibu

    Dembele Yuko poa

    Jibu

    Dembere anajua

    Jibu

    Ni wakati wake sasa kuonyesha cheche zake ndani ya uzi mpya na kumsaidia Suarez katika mbio za kusaka ubingwa La Liga

    Jibu

    Ndo wakati wake sasa

    Jibu

Acha ujumbe