Nyota wa Paris Saint-Germain, Ousmane Dembélé, ameibuka kileleni mwa orodha ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi katika Ligue 1, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na L’Équipe. Dembélé anayeonekana kuwa kwenye kiwango bora, anaingiza euro milioni 1.5 kwa mwezi, kiwango kinachoonyesha nguvu ya kifedha ya PSG.

Kinachovutia zaidi ni jinsi PSG wanavyotawala orodha hiyo, huku nafasi 12 kati ya 15 za juu zikichukuliwa na wachezaji wao. Nahodha Marquinhos anashika nafasi ya pili baada ya Dembélé kwa euro milioni 1.12, akifuatiwa na Achraf Hakimi na Lucas Hernández wanaopata euro milioni 1.1 kila mmoja.
Vipaji chipukizi kama Warren Zaïre-Emery pia vinaonekana kulipwa vizuri, akipokea euro 950,000 kwa mwezi, huku majina kama Vitinha, Khvicha Kvaratskhelia na João Neves yakifunga orodha ya juu kwa euro 900,000 kila mmoja.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mchezaji wa kwanza nje ya PSG kuonekana kwenye orodha hiyo ni Pierre-Emile Højbjerg wa Olympique de Marseille, anayeshika nafasi ya 13 kwa euro 500,000 kwa mwezi, akionyesha tofauti kubwa ya kifedha kati ya PSG na vilabu vingine Ligue 1.

Orodha hii inaweka wazi pengo kubwa la kifedha ndani ya ligi ya Ufaransa, ambapo PSG wanaendelea kutawala si tu uwanjani bali pia kwenye mishahara. Hali hii inaendelea kuzua mjadala kuhusu ushindani wa kweli katika Ligue 1 na uwezo wa vilabu vingine kuendana na kasi ya matajiri hao wa Paris.


