Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps huenda akamkosa Ousmane Dembele kwenye mechi ya Jumapili ya Ligi ya Mataifa dhidi ya Denmark baada ya winga huyo wa Barcelona kupata tatizo kwenye kifundo cha mguu.

 

Deschamps Afichua Kukosekana Leo Dhidi ya Denmark

Mchezo huo utakaopigwa Copenhagen utashuhudia  Deschamps wakifanya mabadiliko kadhaa, safari hiyo inakuja miezi miwili tuu kabla ya timu hizo kukutana tena katika hatua ya makundi ya kundi la Dunia.

Ufaransa wana hamu ya kupata ushindi, kwani hiyo itawakikishia kuepuka kushushwa daraja kutoka daraja la ligi ya Mataifa, lakini kocha huyo hatamsukuma yeyote kucheza. “Ousmane alihisi usumbufu ndani ya mguu na atafanya tofauti” Kocha huyo alisema.

 

Deschamps Afichua Kukosekana Leo Dhidi ya Denmark

Ufaransa na Denmark zitaunganishwa katika kundi D huko Qatar 2022 na Australia na Tunisia, na wanatarajiwa kumanyana Novemba 26 katika mzunguko wa pili wa michezo. Denmark walipata kipigo na Ufaransa kwenye uwanja wa Stade De France mnamo Juni katika mechi yao ya Ligi ya Mataifa, Andreas Cornelius akipiga mara mbili baada ya Kareem Benzema kuwafunga wenyeji.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa