Deschamps Bado Yupo sana Ufaransa

Shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF) limethibitisha kua kocha wa timu hiyo Didier Deschamps ataendelea kusalia ndani ya timu hiyo mpaka kombe la dunia mwaka 2026.

Kocha Deschamps ataendelea kuiongoza timu hiyo mpaka mwaka 2026 licha ya kutupwa nje kwenye michuano ya Euro 2024 jana dhidi ya timu ya taifa ya Uhispania, Hali iliyoleta sintofahamu lakini shirikisho limethibitisha kua kocha huyo ataendelea kuwepo kwenye timu hiyo.deschampsRais wa shirikisho la soka nchini Ufaransa amethibitisha kua kocha huyo ataendelea kuwepo kwenye timu hiyo kwakua yupo ndani ya malengo ambayo walimuwekea, Hivo kwakua yupo ndani ya malengo basi ataendelea kuendelea kukinoa kikosi hicho mpaka mwisho wa mkataba wake ambao ni mwaka 2026.

Kocha Deschamps mpaka sasa ameshatwaa mataji mawili akikinoa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kombe la dunia 2018, na Uefa Nations League 2020, Huku akifanikiwa kucheza fainali tatu mpaka sasa jambo ambalo kwa shirikisho la nchi hiyo wanaona ni moja ya makocha waliofanya vizuri na kikosi hicho miaka ya hivi karibuni.

Acha ujumbe