Luis Diaz aliomba baba yake aachiliwe baada ya kuifungia Liverpool bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Luton.

 

Diaz Aomba Kihisia Kuachiliwa kwa Baba Yake Baada ya Kufunga Bao la Kusawazisha

Baba yake Diaz bado hajapatikana baada ya wazazi wake kutekwa nyara nchini Colombia na mshambuliaji huyo alivua jezi yake kuonyesha ujumbe wa “uhuru kwa baba” baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Harvey Elliott.


Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Alitoa taarifa muda mfupi baada ya mchezo akitaka baba yake aachiliwe.

Diaz Aomba Kihisia Kuachiliwa kwa Baba Yake Baada ya Kufunga Bao la Kusawazisha

Ilisomeka: “baba yangu, ni mtu anayefanya kazi kwa bidii, nguzo ya familia … sasa ametekwa nyara. Naomba ELN [Jeshi la Ukombozi la Kitaifa] kumwachilia baba yangu haraka iwezekanavyo. Pia naomba vyama vya kimataifa vilifanyie kazi hilo ili kumhakikishia uhuru wake.”

Kila sekunde, kila dakika tunakuwa na wasiwasi zaidi. Hatuna maneno ya kuelezea hisia za kutisha za familia yetu, na itakuwa sawa mradi tu hajarudi nyumbani. Nawaomba muachilie baba yangu sasa hivi, kwa kuheshimu uadilifu wake. Nataka kuwashukuru wananchi wote wa Colombia na pia jumuiya ya kimataifa kwa msaada wenu. Ujumbe huo wa Diaz ulisomeka hivyo.

Diaz Aomba Kihisia Kuachiliwa kwa Baba Yake Baada ya Kufunga Bao la Kusawazisha
Klopp aliiambia Sky Sports: “Wakati mzuri sana lakini haibadilishi hali. Jambo muhimu zaidi ni kwamba baba yake aachiliwe. Inashangaza alitaka kuwa hapa. Ni hivyo, kwetu sisi lengo muhimu sana na kwake ni muhimu sana na kihisia, lakini ndivyo hivyo.”

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Klopp alitoa sifa kwa Luton na alikiri timu yake haikustahili pointi tatu akisema kuwa sifa kwa Luton na jinsi walivyolinda na jinsi walivyojipanga lakini ilikuwa juu yao.

Diaz Aomba Kihisia Kuachiliwa kwa Baba Yake Baada ya Kufunga Bao la Kusawazisha

Aliongeza kuwa walikuwa na nafasi nyingi na walipaswa kupata nyingi zaidi. Ni kazi ngumu kusalia kikamilifu.

“Nikiutazama mchezo nadhani hatukustahili zaidi ya pointi moja. Tungeweza kushinda mchezo kwa nafasi tulizopata lakini sasa nikiuangalia nadhani tulistahili pointi.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa